Taasisi za Serikali na binafsi zatakiwa kuwatumia vijana wanao zalishwa vyuoni
10 June 2022, 2:31 pm
Na;Mindi Joseph .
Waziri Ofisi ya Makamu wa Raisi,Muungano na Mazingira Mhe. Selemani Jafo amezitaka taasisi za serikali na binafsi kufungua milango na kuwatumia vijana wanaozalishwa vyuoni ili kujenga umahiri kwa Vijana Nchini
Akizungumza leo katika ufunguzi wa Maonesho ya Elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi amesema Asilimia 56 ya nguvu kazi ni Vijana na Tanzania ina vyou mahiri ambavyo vinazalisha vijana wenye ujuzi.
.
Mtendaji Mkuu Baraza la Elimu ya Ufundi (NACTE) Dkt. Adolf Rutayuga amesema baraza linajukumu la kusimamia elimu na talaama zitolezazo na vyuo.
.
Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa John Kondoro amesema lengo la maonesho haya ni kuonesha ubunifu.
.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema bado serikali inaendelea kuangalia wigo wa kupata mikopo.
.
Kauli mbiu ya Maonesho ya Elimu ya ufundi na Mafunzo ya ufundi stadi “Ni Kuinua Ubora wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa ajili ya Nguvukazi Mahiri Tanzania”