Umbali wa Vitongoji Ovada wachelewesha zoezi la anuani za makazi
9 June 2022, 3:20 pm
Na; Benard Filbert.
Umbali wa vitongoji katika kata ya Ovada wilayani Chemba imetajwa kuwa changamoto iliyosababisha zoezi la anuani za makazi kutokukamilika kwa wakati katika eneo hilo.
Hayo yameelezwa na diwani wa kata ya Ovada Bwana Raphael Reda wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu utekelezaji wa zoezi la anuani za makazi ndani ya kata hiyo.
Amesema changamoto kubwa ni umbali wa makazi ya watu hali iliyosababisha wataalamu kutembea umbali mrefu kwa ajili ya kuwafikia wakazi wa eneo husika.
.
Amesema hadi hivi sasa wamefanikiwa kuweka namba za nyumba pamoja na kutambua barabara za mitaa ambapo hivi sasa wapo katika hatua yakuweka mabango.
Kadhalika amewataka wananchi kutokupinga zoezi hilo na badala yake watoe ushirikiano ili kufanikisha suala hilo kwa maendeleao yakila mmoja.
.
Mfumo wa Anwani za Makazi una manufaa mengikiuchumi, kisiasa na kijamii Katika nyanja za kimataifa,mfumo huu utaifanya Tanzania itambulike vema zaidi.
Usimamizi wa Mwongozo huu ukitekelezwa kwa ufanisiutawezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa kutoa majina ya mitaa, vijiji, njia na barabara kwa usahihi zaidi nakubainisha nambari za nyumba kwa uhakika na hivyo kuwawezesha wananchi kutumia anwani za makazi,jambo ambalo litaongeza tija kwa Serikali na kufanikisha malengo yake ya maendeleo kwa wananchi.