Vyuo vinavyo sajili Bunifu vyatakiwa kuwaendeleza wabunifu
8 June 2022, 1:36 pm
Na;Mindi Joseph .
Vyuo vinavyosajili Bunifu Hapa Nchini na Sekta Binafsi zimeombwa kuendelea kuwawezesha na kuwaendeleza wabunifu ili waweze kuuza kazi zao ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na Taswira ya Habari Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi, Profesa John Kondoro, amesema mbali na serikali kuendelea kufanya jitihadi za kuendeleza bunifu Taasisi binafsi nazo zinatakiwa kuhamasika na kuwawezesha wabunifu ili kutengeneza mifano.
.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi Dkt. Adolf Rutayuga amesema mafunzo yanayotolewa katika vyuo yamekuwa hayana uhusiano na waajiri.
.
Naye Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh Antony Mtaka amevihimiza vyuo vya ufundi kujiongeza na kuwalinda wabunifu na kupitia maonesho hayo wanapaswa kuuza ubunifu.
.
Maonesho ya kwanza ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi mwaka 2022 yanatarajiwa kuzinduliwa na Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango June 10 Jijini Dodoma.