Waziri Jafo ahimiza utunzaji wa msitu wa Iyumbu Park
30 May 2022, 4:45 pm
Na;Mindi Joseph .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Seleman Jafo amesema eneo la msitu la Iyumbu Park likihifadhiwa ipasavyo linaweza kuwa chanzo cha utalii.
Eneo hilo lina zaidi ya hekari 3000 limekuwa eneo maalum lililo tengwa kwaajili ya kupanda miti.
Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa zoezi la upandaji miti katika eneo la msitu la Iyumbu Park ambapo amesema eneo hilo likitunzwa inavyostahili watu wanao kuja Dodoma waweze kujionea utalii uliomo katika eneo hilo.
.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka ameagiza kuwa kila mtu mwenye kiwanja Dodoma kuhakikisha anapanda miti ya matunda na miti ya kuvuli ili kuandoa changamoto za utapiamlo na udumavu unao sababisha kutozingatia lishe bora.
.
Naye, Mkurugenzi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dkt. Andrew Komba amesema miti 441 imepandwa katika eneo hilo huku lengo likiwa ni kupanda miti 3000.
.
Wiki ya Mazingira imezinduliwa Jumamosi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku Mazingira Duniani yanayo tarajiwa kufanyika Juni 5,2022.