Dodoma FM

Wananchi watakiwa kujitokeza kupima shinikizo la damu

17 May 2022, 1:32 pm

Na ;Benard Filbert.

Ikiwa leo ni maadhimisho siku ya shinikizo la damu jamii imetakiwa kujitokeza kupima shinikizo hilo ili kuepusha athari zinazoweza kujitokeza baadaye.

Hayo yameelezwa na daktari Flora Mwakalabo kutoka kituo cha afya makole wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu maadhimisho ya siku ya shinikizo la Damu.

Amesema shinikizo la damu ni nguvu ya msukumo wa damu katika mishipa amabayo inakuwa ni kubwa kuliko kawaida ambapo jamii inatakiwa kuchukua tahadhari kwenda kupima walau mara moja kwa mwaka.

.

Licha ya leo kuadhimishwa kwa siku hiyo imeelezwa bado kunachangamoto ya watu kujitokeza kupima shinikizo la damu kitu ambacho ni hatari kwa afya ya mwanadamu.

Kadhalika amesema kati ya wanaume wanne wanaohudhuria vituo vya afya mmojawapo anakabiliwa na tatizo hilo huku wanawake watano mmojawapo anashinikizo la damu.

.

Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wakazi jijini hapa wamesema elimu itolewe kwa wingi ili kuongeza uelewa wakupima shinikizo la Damu.

Leo ni maadhimisho siku ya shinikizo la damu huku siku hii ikiambatana na kauli mbiu isemayo “KUPIMA SHINIKIZO LA DAMU KWA USAHII KUTHIBITISHA ILI TUISHI MAISHA MAREFU”