Msalaba mwekundu kuadhimisha miaka 60 ya chama chao
6 May 2022, 2:42 pm
Na; Benard Filbert.
Kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya chama cha msalaba mwekundu nchini chama hicho kimepanga kutoa elimu juu ya uviko 19 pamoja na kufanya usafi wa mazingira ikiwa sehemu ya maadhimisho hayo.
Hayo yameelezwa na mratibu wa chama hicho mkoa wa Dodoma bwana Michael Robert wakati akifanya mahojiano na taswira ya habari juu ya maadhimisho ya chama hicho toka kuanzishwa nchini.
Amesema maadhimisho hayo yatafanyika tarehe 8 jijini Dodoma ambapo siku hiyo zitafanyika shughuli mbalimbali ikiwepo kutoa elimu ya uviko 19 pamoja na usafi wa mazingira ambao utafanyika katika hospital ya rufaa mkoa wa Dodoma.
.
Amesema lengo la chama hicho ni kuona watu wengi wanajitokeza katika maadhimisho hayo ili kuongeza uelewa wa jamii kujikinga pindi majanga yanapojitokeza.
.
Naye Geofrey Regnard ni mratibu wa chama cha msalaba mwekundu vyuo vya kati na vyuo vikuu nchini ambapo amesema maadhimisho hayo yatahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu nchi nzima ikihusihwa na visiwani Zanzibar hivyo kila mmoja ajitokeze kupata elimu.
.
Tarehe 8 mwezi may chama cha msalaba mwekundu nchini kinaadhimisha miaka 60 ya chama hicho tangu kuanzishwa nchini lego ikiwa kutoa elimu katika jamii juu ya masuala mbalimbali ya majanga pamoja na afya.