Dodoma FM

Chemba yafikia asilimia 88% Anuani za makazi

2 May 2022, 3:21 pm

Na; Selemani Kodima.

Wakati zoezi la Ukusanyaji wa taarifa za namba za anwani za Makazi likitegemewa kufika Tamati Mei 30, Wilaya ya Chemba imefika lengo katika zoezi la ukusanyaji wa taarifa za anwani za makazi kwa kukusanya taarifa 72958 Sawa na Asilimia 88  huku zoezi la namba likiwa sawa na anwani hizo

Kupitia taarifa hiyo ,Wilaya ya Chemba imefanikiwa katika hatua hiyo kwa Asilimia 100 ya zoezi la Ukusanyaji wa anwani za makazi pamoja na Namba

Akizungumza katika Halfa ya kuwapongeza wakusanyaji taarifa kwa wilaya chemba Mratibu wa Zoezi la Anwani za makazi katika Wilaya Chemba  ambaye pia ni Afisa Ardhi mteule ,Kaimu mkuu wa Idara ya ardhi na Maliasili Bi  Regina Limbumba ametoa taarifa ya zoezi lilivyokwenda katika mafanikio na changamoto ya zoezi la Ukusanyaji wa taarifa hizo .

Amesema zipo kata ambazo zimefanikiwa  na nyingine kukumbwa na changamoto kadhaa ikiwa ni mwanzoni mwa zoezi hilo wakusanyaji taarifa  kukosa Ushirikiano kutoka kwa Viongozi wa serikali za mitaa.

.

kwa upande Mkuu wa Wilaya Chemba Simon Chacha  amewapongeza wakusanyaji wa taarifa  hizo ambao wamefanya zoezi hilo katika kata 26 za wilaya chemba kwa kujituma na kwa bidii licha ya uwepo wa baadhi ya changamoto

Katika Pongezi hizo Mwneyekiti wa Halmashuri ya Chemba  Bw Sambala Said  amewapongeza wakusanyaji taarifa hizo na kusema kuwa yapo mazoezi mengi ambayo yatafanyika hivyo kundi hilo litafirikiwa zaidi .

Wakusanyaji taarifa katika Wilaya ya chemba waliofanya zoezi hilo ni 120 ambapo ziada yao walikuwa watatu wamefanikiwa kupewa Vyeti na Mikataba yenye kutambua mchango wao katika Jukumu hilo ambalo walianza Mwezi mmoja na kufanikiwa kukamilisha haraka  kabla ya tarehe ya mwisho ya zoezi la ukusanyaji wa taarifa za anwani za makazi na namba.