TMA yatakiwa kuweka vipaumbele katika kuboresha huduma
21 April 2022, 3:36 pm
Na;Mindi Joseph .
Waziri wa ujenzi na uchukuzi Prof Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Kuweka vipaumbele zaidi katika kuboresha zaidi huduma zote wanazozitao kwa jamii.
Akizungumza leo jijini Dodoma katika Ufunguzi wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania Prof Mbarawa amesema wizara yake ipo tayari kushirikiana na TMA ili kuboresha zaidi huduma pamoja na masilahi ya wafanyakazi wake.
.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt Agnes Kijazi amesema Sekta ya hali ya hewa imefanikiwa kuongeza usahihi wa utabiri na kufikia wastani wa zaidi ya asilimia 88 ambapo kiwango kinachokumbalika kimataifa ni asilimia 70.
.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya TMA, Dkt. Buruhani Nyenzi amesema changamoto kubwa iliyopo ni watumishi kuhamia taasisi nyingine kutokana na masilahi.
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kimefanyika leo jijini Dodoma na kuwakutanisha wadau mbalimbali katika Kupitia bajeti ya mamlaka ya mwaka 2022/2023 na kufanya tathimini.