Jamii inahitaji zaidi Elimu ya Afya ya akili
7 March 2022, 1:46 pm
Na; Benard Filbert.
Wadau wa afya nchini wameombwa kuwekeza katika utoaji wa elimu ya afya ya akili kwa vijana ili kuwasaidia kuondokana na changamoto mbalimbali.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka wizara ya afya wakati akizungumza na taswira ya habari mara baada ya kufanyika kwa jukwaa la burudani kwa vijana na elimu ya afya ya akili ambalo lililoandaliwa na shirika la Peters Daughter
Amesema moja ya changamoto ambayo imebainika ni kuwa vijana wengi bado hawana uelewa kuhusu afya ya akili hivyo juhudi zinahitajika ili kuongeza uelewa.
CLIP MKURUGENZI…………….01
Hata hivyo amesema maagizo kutoka kwa waziri wa afya Ummy Mwalimu amesema hivi sasa viongozi mbalimbali wa sekta ya afya wawekeze katika kutoa elimu ili kuongeza uelewa.
CLIP 02 MKURUGENZI……………02
Michael Robert ni mratibu wa shirika la msalaba mwekundu katika mkoa wa Dodoma amesema vijana wamekuwa wakijiweka pembeni na suala la afya ya akili na kujikuta katika sintofahamu.
CLIP RED CROSS………………….03
Shirika la Peters Daughter liliandaa jukwaa la burudani na elimu ya afya kwa vijana mkoani hapa lengo ikiwa kutoa elimu katika jamii kutambua afya ya akili.