Ukosefu wa elimu ya huduma ya kwanza wachangia baadhi ya watu kupoteza maisha
21 February 2022, 3:49 pm
Na; Thadei Tesha.
Imeelezwa kuwa ukosefu wa elimu kwa jamii juu ya namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa ni miongoni mwa sababu zinazopelekea baadhi ya watu kupoteza maisha kwa haraka.
Baadhi ya wananchi jijini hapa wamesema ueleewa juu ya suala la kutoa huduma ya kwanza kwa mgonjwa bado upo kwa kiasi kidogo ambapo wamesema ni vyema serikali pamoja na taasisi mbalimbali kuendelea kutoa elimu kwa wingi zaidi juu ya suala hilo.
Aidha wametoa wito kwa walimu pamoja vyombo mbalimbali vya habari kushirikiana na wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu hiyo kwa wingi mashuleni pamoja na jamii kwa ujumla.
Kwa upande wake Daktari Methiew Silayo kutoka katika hospitali ya decca pollyclinic ambaye pia ni muelimishaji wa umma ametoa wito kwa taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyombo vya usafiri kuwa na sanduku la huduma ya kwanza ambapo pia amesesisitiza umuhimu wa kutoa huduma hiyo kwa jamii.
Aidha ameongeza kuwa ni vyema jamii kuendelea kupewa elimu ya kutosha juu ya suala hilo ili kuokoa maisha ya watu kufariki kutokana na kukosa huduma ya kwanza katika jamii.