Mmomonyoko wa maadili waweza kusababisha athari za kisaikolojia
24 January 2022, 2:34 pm
Na ;Thadei Tesha.
Imeelezwa kuwa vitendo vya baadhi ya Watu kuweka picha za utupu mitandaoni zinaweza kuleta athari za kisaikolojia Jambo linalopelekea kuharibika kwa maadili.
Taswira ya habari imefanya mahojiano na baadhi ya vijana jijini hapa kufahamu Nini chanzo cha baadhi ya vijana kuweka picha za utupu kwenye mitandao ya kijamii.
Wamesema baadhi ya visababishi hivyo ni pamoja na vijana wengi kuharibika kimaadili ikiwa ni pamoja na ugeni katika matumizi ya mitandao ya kijamii ambapo wamesema elimu zaidi inahitajika kukomesha vitendo hivyo.
Kwa upande wake mtaalamu wa saikolojia jijini hapa Bw.Muhibu Mtahu amesema picha za utupu mitandaoni zinaweza kuleta athari kisaikolojia Jambo linalopelekea kuharibika kwa maadili katika jamii hivyo jamii pamoja na mamlaka husika zinapaswa kushirikiana kutokomeza vitendo hivyo.
Aidha kwa upande wao baadhi ya wazazi pamoja na viongozi wa Dini wametoa wito kwa vijana kuacha kujihusisha na vitendo hivyo ambapo wamesema wataendelea kuwa mstari wa Mbele kuhimiza maadili katika jamii.