Jamii imetakiwa kuwapa nafasi vijana waliochana na matumiziya dawa za kulevya
18 January 2022, 3:01 pm
Na ; Fred Cheti.
Jamii imeombwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa watu waliochana na matumizi ya dawa za kulevya.
Ikiwemo kuwapatia nafasi katika fursa mablimbali za kimaendeleo kuwasaidia wasiweze kurudi katika matumizi ya dawa hizo.
Wakionekana kuwa na matumaini mapya ya kuanza kupanga upya maisha yao baadhi ya vijana waliokuwa waraibu hapa wanaelezea matamanio yao kwa jamii endapo itaawaamini na kuwapa nafasi tena.
Bw. Christian Mlelwa ni MwanaharakatI kutoka Taasisi ya kupambana na dawa za kulevya ya Wisdom anaelezea nini kifanye kuanzia ngazi ya familia,jamii na serikali ili kumlinda kijna aliyekwisha achana na matumizi ya dawa za kulevya.
Jitihada za Serikali za kupambana na dawa za kulevya zimefanikiwa kupunguza uingizaji wa dawa za kulevya Nchini ambapo kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2019 ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), nchi ya Tanzania ilifanikiwa kupunguza uingizaji wa dawa za kulevya kutoka Nchi zalishaji kwa zaidi ya asilimia 90.