Kongama la tatu la ushiriki wa watanzania katika miradi ya serikali latarajia kufanyika
29 November 2021, 12:33 pm
Na; Mariam Matundu.
Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi linatarajia kufanya kongamano la tatu la ushiriki wa waTanzania katika miradi ya serikali ambalo litakusanya takribani wafanyabiasha 500 ndani na nje ya nchi.
Akizungumza na waandishi wa habari hii leo katibu mtendaji wa baraza hilo Beng’i Issa amesema kupitia kongamano hilo watapata fursa ya kujadili katika maeneo mbalimbali na kujadili changamoto zake.
Clip 1 katibu ………
Amesema licha ya kuwepo kwa watanzania zaidi ya elfu hamsini kuajiriwa katika miradi ya kimkakati hapa nchini bado baadhi ya watanzania wahajaimarika katika ujuzi pamoja na uhaba wa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.
Clip 2 katibu………
Aidha amewataka vijana kuchangamkia fursa katika sekta ya kilimo kwakuwa malghafi nyingi za viwandani zinatokana na kilimo.
Clip 3 katibu…………
Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika dec 13 na 14 mwaka huu Dar Es Salaam ambapo mgeni rasmi atakuwa waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa na kauli mbiu ikiwa ni WEZESHA USHIRIKI WA WATANZANI .