Serikali imewataka wananchi walio omba vitambulisho vya Taifa kwenda ofisi za usajili za wilaya , kata na vijiji.
26 November 2021, 1:38 pm
Na; Fred Cheti .
Serikali imewataka wananchi wote walioomba vitambulisho vya Taifa kwenda katika ofisi za Usajili za wilaya ,kata pamoja na vijini walipofanya usajili kwa ajili ya kwenda kuchukua vitambulisho hivyo badala ya kulalamika kuwa vitambulisho hivyo havitoki.
Wito huo umetolewa leo na waziri wa mambo ya ndani Mh. Goerge Simbachawene wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa juu ya mafanikio na mikakati ya wizara hiyo ambapo amesema kuwa licha ya mamlaka kuzalisha vitambulisho vichache bado jumla ya vitambulisho 1,103,882 bado havichachukuliwa hivyo ni vyema wananchi wakafika katika ofsi hizo kwa ajili ya kupatiwa.
Katika hatua nyingine waziri Simbachawane amesema kuwa wizara imeendelea kuboresha miundombinu katika baadhi ya sekta ndani ya wizara hiyo ikiwemo ya idara ya uhamiaji pamoja na jeshi la zimamoto nchini huku akiwataka wananchi kuendelea kuzingatia sheria pamoja na kutoa ushirikiano katika vyombo hivyo.
Baadhi ya wananchi jijijin hapa wakitoa maoni yao juu ya suala hilo wamesema mlolongo katika ufuatiliaji wa vitambulisho hivyo ndio sababu inayowafanya watu wengi kutokua na muamko katika uchukuaji wa vitambushio hivyo
Serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani imeendelea kuboresha ulinzi kwa wananchi kwa kuimarisha utendaji kazi katika sekta ya uhamiaji , jeshi la zimamoto nchini pamoja Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa amabayo imeendelea na jukumu la usajili na utambuzi wa watu kwa kugawa vitambulisho
.