Kukosekana kwa utu ni chanzo cha kushamiri kwa biashara ya dawa za kulevya
22 October 2021, 12:27 pm
Na; Fred Cheti.
Kukosekana kwa utu inatajwa kuwa chanzo cha kushamiri kwa biashara ya dawa za kulevya duniani kote kwa kua biashara hiyo inatajwa kudhalilisha utu na heshima ya binadamu.
Hii ni kulingana na shirika la habari la kidini la VATICAN NEWS ambalo linaeleza kuwa biashara hiyo imekuwa ikifanywa na watu wenye uchu wa mali na utajiri wa haraka kiasi cha kushindwa kuona madhara yake katika ustawi,maendeleo na mafao ya wengi
Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi zinazokabiliana na janga hili la matumizi ya dawa za kulevya taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wakazi jijini hapa kutaka kufahamau namna gani jamii inaweza ikashiriki katika kuunga juhudi za serikali katika mapambano dhidi ya janga hilo.
Kwa upande wake mtoa elimu kuhusiana na madhara ya dawa hizo Bw. Christian Mlelwa kutoka katika kliniki ya wisdom anasema kuwa mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa hizo yanaanza katika ngazi ya familia endapo wazazi au walezi watasimama vizuri katika malezi ya mtoto watapunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya mtoto kujiingiza katika matumizi na biashara ya dawa hizo.
Matumizi haramu ya dawa za kulevya ni donda wazi katika jamii nyingi na madhara yake yanajionesha hata kwenye familia na jamii husika! hivyo serikali pamoja na wadau mbali mbali wanapaswa kuunganisha nguvu ili kufanya upembuzi yakinifu katika mapambano juu janga la matumizi haramu ya dawa za kulevya,