Wiki ya AZAKI kuanza kesho
22 October 2021, 12:06 pm
Na;Mindi Joseph.
Ikiwa kesho ni Wiki ya Asasi za kiraia nchini AZAKI imetajwa kukua zaidi na kuchangia maendeleo endelevu nchini pamoja na wananchi.
Akizungumza leo jijini Dodoma Nesia Mahenge Mkurungezi Mkazi CBM Tanzania amesema kila kwenye maendeleo ya nchi AZAKI imeshiriki kwa kiasi kikubwa.
Ameongeza kuwa asasi zote za Kiraia nchini zinakutana kwenye wiki ya AZAKI ambayo itaanza kesho na itahusha matukio mbalimbali huku mgeni Rasmi akiwa ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Job Ndugai.
Kwa upande wake Mkurungezi Mtendaji wa shirika la umoja wa mataifa Tanzania UNA Reynald Maeda amebainisha kuwa washiriki zaidi ya miatano watashiriki katika majadiliano ambayo yatafanyika kuanzia octoba 25-28.
Wiki ya AZAKI Nchini imeanza kufanyika mwaka 2018, ili kusaidia wananchi kupata uelewa mpana kuhusu kazi zinazofanywa na Azaki mbalimbali nchini na mwaka huu wiki hiyo inabebwa na Kauli Mbiu isemayo “Azaki na Maendeleo”