Walimu waadhimisha siku ya mwalimu kwa kuomba kuboreshewa mazingira ya kujikinga na uviko 19
5 October 2021, 10:53 am
Na; Selemani Kodima.
Ikiwa leo ni siku ya walimu Dunia ,Baadhi ya walimu wamesema ipo haja ya kundi hilo kutazamwa zaidi katika namna ya kujikinga na Ugonjwa uviko-19 kutokana na mazingira ya ufundishaji kuhusisha watu wengi .
Hayo yamesemwa na baadhi ya walimu wakati wakitoa maoni yao kuhusu siku ya walimu duniani ambapo wameainisha changamoto zinazowakabili kwa sasa katika kukabiliana na Janga la Uviko 19 katika mazingira ya kazi.
Ally Ramadhani ni Afisa Elimu kata ya Matumbulu mkoani Dodoma amesema ni muda muafaka walimu kuchanja chanjo ya Uviko-19 ili kuwa salama zaidi kutokana na mazingira ya kazi zao.
Nae Mwalimu Bakari Mtembo amesema ili kuwasaidia walimu kuwa na ufahamu wa Janga hilo haina budi wapewa semina na mafunzo kuhusu namna ya kujikinga na kutengeneza mazingira rafiki wakati wa Ufundishaji.
Hata Hivyo amesema kupitia Walimu inaweza kusaidia kufikisha Elimu kwa Jamii juu ya Janga la uviko-19 pamoja na umuhimu wa chanjo kwa Jamii.
Leo ni siku ya walimu Dunia ambapo , umoja wa mataifa UN uliteua terehe 05/oktoba kuwa siku muhimu zaidi kwa walimu wote kwasababu ndio siku ambayo 05/10/1966,,umoja wa mataifa ulipitisha sheria mbili.