Jamii yaaswa kuacha kutupa ovyo barakoa zilizo tumika
21 September 2021, 12:51 pm
Na; Benard Filbert.
Jamii imetakiwa kuacha kutupa hovyo barakoa zilizotumika ili kuepuka kusababisha magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya hewa.
Hayo yameelezwa na afisa afya wa jiji la Dodoma Abdallah Mahiya wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu athari za utupaji hovyo wa barakoa zilizotumika.
Amesema jamii inatakiwa kutambua kuwa barakoa zilizotumia zinatakiwa kuhifadhiwa katika vyombo maalumu na sio kutupa pasipo utaratibu maalumu.
Amesema sehemu ambazo kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu za kutupa barakoa huenda wananchi hao hawana elimu ya kutosha hivyo ni wajibu wa kila mtu kutoa elimu juu ya athari za barakoa zilizotumika.
Baadhi ya wananchi wameiambia taswira ya habari kuwa ni vyema kila mmoja akahifadhi vizuri kwenye vyombo vya kuhifadhia takataka ili kuepuka watoto kuzivaa tena.
Halmashauri ya jiji la Dodoma kwa kushirikiana na wataalamu wa afya wamekuwa wakihamasisha jamii kuhusu kuhifadhi vyema barakoa zilizotumiaka il kuepuka watoto kuzivaa hali inayoweza kusababisha kusambaa kwa magonjwa.