Dodoma FM

Dawati la jinsia Dodoma lasema hakuna tukio la ndoa za utotoni lililo ripotiwa tangu january hadi Agost 2021

1 September 2021, 12:11 pm

Na;Mariam Matundu.

Imeelezwa kuwa kwa kipindi cha miezi nane tangu januari mpaka Agost mwaka huu 2021 hakuna tukio la ndoa za utotoni lililo ripotiwa dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Dodoma Mjini .

Hayo yamesemwa na mkaguzi msaidizi wa polisi dawati la jinsia Jelda Luyangi ambapo amesema kuwa hiyo inaleta tafsiri nyingi kwamba huwenda matukio yanafanyika kwa siri kubwa au huwenda jamii imeachana na mila hizo.

Aidha ametoa rai kwa mabinti kuwa makini pale wanapo ona dalili za kutaka kuozeshwa katika umri mdogo kufika katika ofisi za dawati la jinsia ili kutoa taarifa na kuwachukulia wazazi hatua.

Nae afisa vijana kutoka taasisi ya maendeleo ya vijana Dodoma DOYODO Bw. Adamu Cosmas amesema wamekuwa wakitoa elimu katika shule mbalimbali na kuwajengea uwezo wasichana ili kuweza kupiga vitendo hivyo pindi vinapotokea.

Kwa mjibu wa utafiti wa Demografia y afy Nchini (tdhs) wa mwaka 2010 mikoa yenye viwango vikubwa vya ueneaji wa ndoa za utotoni hapa Nchini ni pamoja na Shinyanga, (59%), tabora (58%), Mara (55) na Dodoma (51%) hii ikiwa ni sawa na wastani wa wasichana wawili kati ya watano huolewa kabla hawajatimiza umri wa miaka 18.