Serikali kuongeza jitihada ya kutatua changamoto za wafanyakazi Nchini
25 August 2021, 12:42 pm
Na;Mindi Joseph.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa amesema serikali itaongeza jitihada za kutatua changamoto zinazowakabili wafanyakazi nchini.
Akizungumza leo jijini Dodoma wakati wa kufungua mkutano wa chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania TALGWU Waziri Majaliwa amesema serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na chama hivyo inaendelea kufanyia kazi changamoto hizo ikiwa ni pamoja kuanza kulipa mafao ya watumishi waliostaafu.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amewataka waajiri wote nchini kuhakikisha wanazingatia wajibu wa kuratibu na kuwasilisha michongo ya watumishi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii ili kuondoa migogoro isiyositahili.
Awali akizungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama,amesema vyama vya wafanyakazi vinatakiwa kuwa nguzo na kuunganisha wafanyakazi pamoja na kuwawakilisha katika mashauri mbalimbali yanayoondoa ustawi.
Naye Katibu mkuu wa chama chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa Tanzania TALGWU Bw,Rashid Mtima amemuomba Waziri Mkuu kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi nchini ikiwemo watumishi wanaostafu kucheleweshewa kulipwa mafao yao kwa mujibu wa sheria.
Mkutano wa 8 wa chama cha TALGWU umefunguliwa rasmi leo jijini Dodoma na Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa.