Familia zatakiwa kuvunja ukimya juu ya hedhi salama kwa mtoto wa kike
23 August 2021, 1:40 pm
Na; Mariam Matundu.
Imeelezwa kuwa ili kuvunja ukimya na kuwezesha upatikanaji wa hedhi salama kwa watoto wa kike ni muhimu suala hili likaanza kuzungumzwa ndani ya familia pamoja na kujumuishwa kwenye bajeti za familia.
Akizungumza na taswira ya habari mdau wa masuala ya hedhi Japhet Jackson amesema wanaume kutokushirikiswa suala ya hedhi kunaathiri upatikanaji wa huduma bora za hedhi salama.
Aidha amesema ni muhimu wadau wakaongeza juhudi katika kuelimisha jamii ili kuondoa mila na desturi potofu juu ya suala ya hedhi .
Taswira ya habari imezungumza na baadhi ya wananchi kutaka kujua ni kwa namna gani wanahakikisha hedhi salama kwa mtoto wa kike ambapo bado kunaimani potofu juu hedhi.
Jamii bado inafanya suala la hedhi kuwa la kificho na aibu kuzunguzwa hadharani hivyo bado wadau wanahitaji kuongeza nguvu katika kutoa elimu hii ya hedhi.