Wafanyabiashara waliopo mnada wa Dabalo wametakiwa kufuata taratibu ili kujikinga na uviko 19
22 July 2021, 8:45 am
Na; Benard Filbert.
Wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali wanaofanya shughuli zao katika mnada wa Dabalo wilaya ya Chamwino wametakiwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma kila mmoja kuvaa barakoa na kuzingatia kuweka maji ya kunawa ili kujikinga na Corona.
Hayo yameelezwa na diwani wa kata ya Dabalo bwana Isihaka Rajab wakati akizungumza na taswira ya habari kuhusu utekelezaji wa maagizo ya mkuu wa mkoa Anthony Mtaka kuhusu kila mfanyabiashara kwenye minada kuvaa barakoa.
Amesema maagizo hayo yanafanyiwa kazi lakini kata ya Dabalo imeandaa mafudi maalum ambao wanatengeneza barakoa hivyo kuanzia mnada ujao kila mtu atakuwa na barakoa pamoja na vifa vya kunawia .
Amekiri kuwa kata hiyo haina elimu ya kutosha kuhusu kujikinga na virusi vya corona hivyo wamewekeza katika suala la utoaji wa elimu ambapo hivi sasa wameanza kuzunguka kila kijiji kuelimisha jamii.
Hivi karibuni mkuu wa mkoa wa Dodoma Antony Mtaka akiwa katika utatuizi wa migogoro y ardhi michese alitoa maagizo kwa wafanyabiashara wote maeneo ya minada kuhakikisha wanachukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa wa corona ikiwemo kuvaa barakoa kwani maeneo hayo yanakuwa na mikusanyiko ya watu wengi.
Jamii imeendelea kukumbushwa kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na corona ikiwepo kuvaa barakoa sehemu zenye mikusanyiko.