Wizi wapelekea wakazi wa Makulu kuishi bila amani
24 May 2021, 10:16 am
Na; Benjamin Jackson.
Wakazi wa kata ya Makulu Jijini Dodoma wamelalamikia eneo hilo kukumbwa na wimbi la wizi hali inayopelekea wananchi kukosa amani katika makazi yao.
Wakizungumza na Dodoma fm wananchi hao wamesema tatizo la wizi katika eneo hilo limekuwepo kwa muda mrefu lakini hakuna hatua zozote zinazo chukuliwa na uongozi wa eneo hilo hivyo wameiomba serikali isaidie kutatua changamoto hiyo.
Taswira ya habari ilizungumza na mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Leonard Ndama ambapo amethibitisha kuwepo kwa wizi wa vitu mbali katika eneo hilo hivyo amewataka wakazi wa eneo hilo kuwa makini na mali zao .
Bw . Ndama amesema swala la ulinzi shirikishi limekuwa likishindikana katika eneo hilo kutokana na kukosekana kwa pesa za kuwalipa watu wanao jitolea kufanya doria katika mitaa ya kata hiyo hivyo amewaomba wananchi wakubali kuchangia pesa hizo.
Nae Diwani wa kata hiyo Bw ..Fadhili Chibago amesema tayari amekwisha zungumza na wenyeviti wa mtaa ili kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi na amewataka vijana wanao jihusisha na tabia za wizi katika eneo hilo kuacha mara moja badala yake wajiunge kwenye vikundi mbalimbali ili wapate mikopo itakayo wawezesha kujikwamua kiuchumi.