Wananchi watakiwa kufuatili na kuhoji miradi ambayo imekamilika na haitumiki
12 May 2021, 12:47 pm
Na; Mindi Joseph
Serikali imehimizwa kuwashirikisha wananchi katika ujenzi wa miradi ya maendeleo ili kuokoa hasara inayojitokeza kufuatia asilimia 36 ya miradi iliyokamilika Nchini kutotumika licha ya kugharimu rasilimali nyingi za fedha.
Taswira ya habari imezungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga ambaye amesema kwa mujibu wa Taarifa ya mwaka wa fedha 2019/2020 imeonyesha kuwa miradi mingi iliyokamilika nchini imekuwa haitumiki ipasavyo ili kuwanufaisha wananchi. Ameongeza kuwa nguvu kubwa inahitajika kutoka kwa wananchi katika kufuatili na kuhoji juu ya miradi iliyokamilika na haitumiki.
Kwa upande wake Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mstaafu Ludovick Utouh ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Wajibu ameainisha kuwa miradi mingi inatekelezwa nchini na kukamilika kwa kutumia pesa za watanzania lakini haitumiki.
Taasisi ya Foundation For Civil Society (FCS) kwa kushirikiana na taasisi ya wajibu leo imeketi jijini dodoma na Jukwaa la wakurungezi wa Taasisi mbalimbali za Kiraia kujadili kuhusu taarifa ya ukaguzi wa hesabu za serikali ili kuongeza uwajibikaji na kuimarisha utendaji wa serikali na udhibiti wa rasimali za nchi.