Elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia imesaidia kuondoa ukimya kwa jamii
3 May 2021, 1:37 pm
Na; Mindi Joseph
Imeelezwa kuwa elimu ya kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto imechangia wengi kuripoti hususani watoto wa kike katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Taswira ya Habari imezungumza Askari polisi wa Dawati la jinsia ,wanawake na watoto kituo cha polisi Wilayani Mpwapwa Shafii kawalata amebainisha kuwa Elimu hiyo imewezesha watu wengi kufahamu namna ya kuripoti vitendo hivyo ambavyo hurudisha nyuma maendeleo ya jamii.
Ameongeza kuwa mmomonyoko wa maadili kwa wazazi imekuwa chanzo cha watoto kukumbwa na ukatili wa kijinsia na wanajitahidi wakichukua hatua za awali ili kumsaidia muathirika wa vitendo hivyo .
Aidha baadhi ya wananchi wamekiri kuripoti vitendo vya ukatili kutokana elimu ambayo wamekuwa wakiipata kutoka kwa wadau mbalimbali wa kupinga ukatili.
Ukatili wa kijinsia ni ukiukwaji mkubwa wa Haki za Msingi za Binadamu na una madhara ya muda mrefu ya kimwili, kiakili na kisaikolojia kwa watu waliopatwa.