Uongozi wa kata ya Mnadani waahidi kutatua kero ya barabara
26 April 2021, 7:03 am
Na; Alfred Bulahya
Wananchi wa kata ya Mnadani jijini Dodoma wametakiwa kutoa ushirikiano pamoja na kuwa wavumilivu, wakati uongozi wa kata hiyo ukifanya jitihada za kutatua kero ya ubovu wa miuno mbinu ya barabara za mtaa ili kusaidia kufanikisha zoezi hilo.
Hayo yamebainishwa leo na Diwani wa kata ya Mnadani Bw, Paul Richard wakati akizungumza na taswira ya habari na kusema kuwa uongozi unatambua uwepo wa changamoto hiyo.
Amesema kwa sasa jitihada kubwa zinaendelea kufanyika ili kuanza ukarabati wa barabara hizo ikiwemo barabara ya Usomalini ambayo imekuwa kero kwa watumiaji kwa kipindi cha muda mrefu.
Amesema ni kweli barabara ya usomalini imekuwa ikiwafanya watumiaji kushindwa kupita kwenda kufanya shughuli zao za maendeleo huku wakazi wa ndachi wakikosa usafiri kutokana na baadhi ya wamiliki wa vyombo vya usafiri kuhofia kuharibika.
Pamoja na hayo amewataka wananchi hao kutoa ushirikiano wa kutoka wakati zoezi la ujenzi na ukarabati litakapoanza.