Jamii imetakiwa kujali na kuwathamini watoto wanao ishi na kufanya kazi mtaani
14 April 2021, 9:48 am
Na Mariam Kasawa
Imeelezwa kuwa mtoto anae ishi mtaani ana haki ya kupata haki zote za msingi kama anazopatiwa mtoto mwingine ili kumkinga na maovu.
Akizungumza na Kapu kubwa la Dodoma fm Afisa ustawi wa jamii ngazi ya mtaani wa shirika la KISEDET Bw. Ibrahim Mtangoo amesema shirika lao linaadhimisha siku ya mtoto anae ishi na kufanya kazi mtaani leo Aprili 14 wakiwa na lengo la kuifahamisha jamii kuwa mtoto anae ishi na kufanya kazi mitaani ana haki sawa na watoto wengine hivyo anapaswa kupewa haki zote za msingi anazo pewa mtoto.
Bw. Ibrahim amesema kuwa ni vema jamii na serikali kupaza sauti kwamba watoto wanao ishi na kufanya kazi mtaani hawana tofauti na watoto wengine ila kuna sababu zilichangia watoto hao kwenda kuishi mtaani ikiwemo matatizo ya kifamilia, wazazi, jamii na hali ya uchumi katika familia.
Amesema watoto wanaoishi mtaani wanapitia maisha magumu ikiwa ni pamoja na kukosa haki nyingi ikiwemo haki ya kupata elimu , haki ya kulindwa na usalama wao pia haki ya kukosa matibabu pale wanapo ugua hali inayopelekea baadhi yao kupoteza maisha, pia watoto wamekuwa wakipitia manyanyaso kupitia kwa watu wengine kama kupigwa na kuonewa bila kupatiwa msaada wowote na jamii .
Aidha ameitaka jamii isiwatenge watoto wanao ishi mtaani kwa kuhakikisha wanawasaidia watoto hawa kurudi katika njia sahihi na kuwaepusha na mambo maovu.
Siku ya mtoto anae ishi na kufanya kazi mtaani huadhimishwa kila April 12 lakini kwa mkoa wa Dodoma Shirika la KISEDETI limeadhimisha siku hiyo leo Aprili 14 huku maadhimisho hayo yakiwa yamebabe kaulimbiu inayo sema “ Mtoto anae ishi na kufanya kazi mtaani anahaki sawa na watoto wengine .