Rais mh.Samia Suluhu ashiriki dua maalum ya kumuombea hayati rais amani abeid karume
7 April 2021, 1:09 pm
Na; Mariam Matundu
Ikiwa leo ni kumbukumbu ya kifo cha rais wa awamu ya kwanza wa Zanzibar hayati Abedi Amani Karume, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan ameshiriki dua maalum ya kumuombea iliyofanyika visiwani humo.
Katika dua hiyo maalumu iliyofanyika katika viwanja vya CCM Kisiwandui mahali alipozikwa hayati Karume , mjumbe wa baraza la ulamaa Zanzibar Shekhe Shaabani Salim Batashi mbali na kuongoza dua hiyo amesisitiza kuendelea kuzungumza mambo mazuri yaliyofanywa na watu waliotangulia mbele za haki.
Wakazi wa Zanzibar wamemuelezea hayati Abeid Karume kwamba alikuwa mzalendo na alipenda kushirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo ya nchi yake .
Hapa Tazania bara wachambuzi wa masuala ya siasa wanasema ni vizuri kufundisha Historia ya masuala mbalimbali ya Tanzania ili kuendelea kudumisha na kuzipa thamani kumbukumbu za viongozi mbalimbali.
Ni miaka 49 tangu kifo cha hayati Abed Amani Karume ambapo hii leo imetumika kumuombea dua maalumu iliyohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali na dini wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan , Rais wa Zanzibar Hussen Ally Mwinyi na waziri mkuu wa Tanzania Kassimu Majaliwa.