Serikali kuwatambua watoa mikopo ya kilimo
31 March 2021, 9:17 am
Na; Mariam Matundu
Kutokana na changamoto ya baadhi ya wakulima kushindwa kupata mikopo ya pembejeo kwasababu ya riba kubwa na masharti mengine yanayotolewa na watoa mikopo, serikali kupitia wizara ya kilimo imeanza kuwatambua watoa huduma wote wanaotoa mikopo ya kilimo.
Akizungumza leo bungeni wakati akijibu swali la mbunge wa Nkasi Aida Kenani Naibu Waziri wa kilimo Hussen Bashe amesema hatua hiyo itasaidia kutambua changamoto zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi .
Aidha amesema kwa mwaka 2020 /2021 hadi mwezi february mfuko wa taifa wa pembejeo umetoa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 959 na laki tano ikiwemo mikopo ya matrekta makubwa 62 yenye thamani ya sh billion 5.6.
Wakati huo huo mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole aliuliza serikali inamkakati gani katika kuongeza uzalishaji wa maharage ya soya ambayo Tanzania imeingia mkataba na China kupeleka takribani tani laki 4 kwa mwaka ambapo uzalishaji kwa Tanzania bado upo chini.
Akijibu swali hilo Naibu waziri Hesseni Bashe amesema tayari tani 140 zimesafirishwa mwezi march na kuongeza kuwa wizara imechukua hatua ili kuongeza uzalishaji wa mbegu ikiwa ni pamoja na kutenga fedha ya kuwezesha mashamba ya ASA.