Maabara bubu zatakiwa kujisajili hadi kufikia aprili 30
31 March 2021, 6:25 am
Na ; Mariam kasawa
Wamiliki wa Maabara bubu Nchini ambazo hazijasajiliwa wamepewa kipindi cha mwezi mmoja kuanzia leo hadi Aprili 30 wawe wamesajili Maabara zao ili kuepuka kufungiwa.
Agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe wakati wa mkutano na Wamiliki wa Maabara binafsi za Mkoa wa Dar Es Salaam wenye kauli mbiu isemayo “Ushirikiano wa Wadau ni nguzo Muhimu katika utoaji wa Huduma Bora za Afya” uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Mwalimu Nyerere mkoani humo.
Dkt. Grace amesema kumekua na ongezeko kubwa la Maabara bubu Nchini ambazo nyingine zinafunguliwa katika makazi ya watu na kusababisha kuhatarisha Maisha ya watu wanaokaa maeneo hayo hususani Watoto ambao wana tabia ya kuchezea vitu hatarishi.