Wanawake wategemea ardhi kujipatia kipato
19 March 2021, 12:30 pm
Na, Alfred Bulahya.
Imeelezwa kuwa wanawake zaidi ya asilimia 50% wanategemea ardhi kwaajili ya kipato chao, Kauli hiyo imetolewa na Kamishna Ustawi wa jamii Dkt Naftali Ng’ondi jijini Dodoma wakati akifungua mkutano uliokuwa ukifanyika kwa njia ya mtandao ambao umehusisha Nchi wanachama wa UN zaidi ya 140.
Amesema uelewa na muamko wa wanawake bado ni mdogo katika Nchi ya Tanzania huku akisema Serikali imeweka mkakati madhubuti wa kuhamasisha kutambua umuhimu wa kumiliki ardhi na kuongeza kuwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka wazi kila mwananchi ana haki ya kumiliki ardhi bila kujali jinsia yake.
Mboni Mgaza ni kaimu mkurugenzi Idara ya Maendeleo Jinsia chini ya Wizara ya Afya Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii amesema ,Wizara pamoja na majukumu mengine imepewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa sera ya wanawake na jinsia.
Mkutano huo hufanyika kila mwaka ambao hutoa fursa kwa wataalamu wanaohusika na afua mbalimbali za utekelezaji kwa ajili ya kuleta usawa wa kijinsia na kujadiliana juu ya mafaniko ambayo yamepatikana katika utekelezaji wa sera,sheria pamoja na mipango mengine.