Dodoma FM

Mvua zakwamisha ukarabati miundombinu ya maji

25 February 2021, 6:46 am

Na,Benard Philbert,

Dodoma.

Mvua zinazoendelea kunyesha nchini zimetajwa kuwa kikwazo cha kutokukamilika kwa marekebisho ya miundombinu ya maji katika mtaa wa Mahomanyika jijini Dodoma.

Miezi mitatu iliyopita baadhi ya wakazi wa mtaa huo walinukuliwa wakilalamika ukosefuwa huduma ya maji kutokana na miundombinu hiyo kutokuwa imara hivyo kushindwa kuhimili kiwango cha maji.

Akizungumza na taswira ya habari mwenyekiti wa mtaa huo Bw.Ernest Kutona amesema tayari wamefikia muafaka na wakala wa maji na usafi wa mazingira Vijijini RUWASA kuhusu kukarabati miundombinu hiyo ili huduma ya maji irejee ila mvua ndio inayokwamisha ukarabati huo.

Amesema mvua hiyo imeleta athari kubwa ikiwepo kusababisha kuzama kwa mashine ambayo inavuta maji kwenye kisima na kusambaza kwa wananchi.

Amewataka kuwa wavumilivu wakati wanasubiri utatuzi wa changamoto hiyo kwani lengo ni kila mwananchi apate huduma ya maji safi na salama.
Na Benard Filbert.