Dodoma FM

Vipigo kwa wanawake kukomeshwa ifikapo 2022

29 January 2021, 9:56 am

Na,Mindi Joseph,

Dodoma.

Serikali imesema itaendelea kuhakikisha changamoto ya wanawake kufanyiwa ukatili kwa kupigwa inapungua kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Taswira ya habari imezungumza na Monika Chisongela Mratibu wa Dawati la Jinsia Wilaya ya Bahi, ambapo amebainisha kuwa jumla ya visa 219 vya wanawake kupigwa vimeripotiwa Polisi mwaka 2020 hivyo Serikali inaendeleza juhudi za kuhakikisha haki za wanawake zinalindwa.

Kwa upande wake Mratibu wa Shirika la Surungai Paralegal lililopo Wilayani Bahi, Tumaini Chuga amesema wanaendelea kuifikia jamii na kutoa elimu juu ya athari za kumpiga mwanamke kwani baadhi yao wanajeruhiwa na wengine kupoteza maisha.

Katika ripoti ya haki za binadamu Tanzania iliyotolewa mwaka 2019 na kituo cha sheria na haki za binadamu(LHRC), wanawake 80,000 wamefanyiwa ukatili nyumbani kuanzia mwaka 2017 na ukatili huu ulisababisha vifo kwa baadhi yao.