Dodoma FM

TAREWU kuwakutanisha washirika ukusanyaji mapato januari 15-16 Dodoma

14 January 2026, 5:39 pm

 Picha ni Katibu Mkuu wa TAREWU, Michael Marere, akiongea na waandishi wa habari kuhusu mkutano huo.Picha na TAREWU.

TAREWU imesisitiza kuwa mkutano huo ni sehemu ya mkakati wa chama katika kuimarisha mshikamano, elimu kwa jamii na mchango wa wafanyakazi wa ukusanyaji mapato katika maendeleo ya nchi.

Na Anwary Shaban.

Chama cha Wafanyakazi wa Kukusanya Mapato Tanzania (TAREWU) kimetoa wito kwa umma, wadau na washirika wake kushiriki mkutano mkubwa wa chama hicho unaotarajia kufanyika januari 15 hadi 16, katika Ukumbi wa Sephill Sephire, jijini Dodoma.

Mkutano huo ambao unalenga kuwakutanisha wanachama, wadau na washirika wa sekta ya ukusanyaji wa mapato, utaambatana na matukio matatu muhimu, ikiwemo mbio za mshikamano, tukio linalotarajiwa kuwakutanisha wananchi wa makundi mbalimbali.

Akizungumza na Taswira ya Habari, Elias Manyama, ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TAREWU, amesema kuwa lengo kuu la mbio za mshikamano ni kutoa elimu kwa wafanyabiashara nawajasiriamali, hususan kuhusu umuhimu wa kushiriki katika shughuli halali za kiuchumi na ulipaji sahihi wa kodi kwa maendeleo ya taifa.

Sauti ya Elias Manyama

Aidha, Bw. Elias mewataka wafanyabiashara na wajasiriamali jijini Dodoma na maeneo ya jirani kujumuika kikamilifu katika mkutano huo, wakibeba bidhaa na huduma zao, ili kujipatia kipato na kupanua wigo wa biashara zao kupitia fursa zitakazopatikana wakati wa mkutano.

Amesema hatua hiyo itasaidia sio tu kuinua uchumi wa wafanyabiashara binafsi, bali pia kukuza uchumi wa Jiji la Dodoma kwa ujumla, sambamba na kuimarisha ushirikiano kati ya TAREWU, wanachama na jamii.

Sauti ya Elias Manyama