Dodoma FM

Yapi mazingira rafiki kwa wenye ulemavu kushiriki uchaguzi?

11 September 2025, 4:43 pm

Tanzania ina takriban watu milioni 5.3 wenye ulemavu, sawa na asilimia 11.2 ya Watanzania wote.Picha na Full shangwe.

Sheria ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 inatambua haki ya kushiriki katika maisha ya kisiasa, ikiwemo kupiga kura na kugombea nafasi za uongozi.

Na Yussuph Hassan.
Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, wadau wa haki za watu wenye ulemavu wameendelea kutoa wito kwa serikali na Tume Huru ya Uchaguzi pamoja na vyama vya siasa kuhakikisha mazingira ya uchaguzi yanakuwa jumuishi na rafiki kwa watu wenye ulemavu.

Wito huo unalenga kuhakikisha kuwa kundi hilo linashiriki kikamilifu katika mchakato wa kidemokrasia bila vikwazo vya kimazingira au kijamii.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, Tanzania ina takriban watu milioni 5.3 wenye ulemavu, sawa na asilimia 11.2 ya Watanzania wote.

Takwimu hizo zinaonyesha kuwa wanawake wenye ulemavu ni asilimia 11.6, huku wanaume wakiwa asilimia 10.9.

Aidha aina ya ulemavu unaoongoza ni wa macho, ukichukua asilimia 3.6 ya jumla ya watu wenye ulemavu.

Lakini baadhi ya watu wenye ulemavu wamekuwa wakielezea namna wanavyoona mazingira yalivyo hasa wakati huu kampeni za uchaguzi zikiwa zinaendelea kuwa bado haziwapi nafasi ya kujua sera na Vipaumbele vya wagombea.

Aidha, Sera ya Taifa ya Maendeleo na Huduma kwa Watu Wenye Ulemavu ya mwaka 2004 inasisitiza ushirikishwaji wa kundi hili katika mipango ya maendeleo ya taifa.

Said Hamis ni kijana mwenye ualbino tumefanya naye mazungumzo kufahamu mazingira rafiki ni yapi ili watu wenye ulemavu washiriki katika uchaguzi mkuu. Sikiliza zaidi.