Dodoma FM
Dodoma FM
3 July 2025, 3:47 pm

Katika kufahamu suala hili, Selemani Kodima mapema alifika hadi Wilaya ya Kondoa na kutuandalia taarifa ifutayo.
Na Seleman Kodima.
Katika mwaka 2025, hali ya mimba za utotoni imeendelea kuwa changamoto kubwa duniani, hususan katika nchi zinazoendelea, lakini pia kuna maendeleo yanayoleta matumaini.
Wasichana milioni 16 wenye umri wa miaka 15–19 na milioni 2 walio chini ya miaka 15 hujifungua kila mwaka.
Asilimia 95 ya mimba hizi hutokea katika nchi za kipato cha chini na cha kati, hasa vijijini na kwenye jamii zisizo na elimu ya kutosha.
WHO imetoa mwongozo mpya wa kimataifa unaolenga kuzuia mimba za utotoni kwa njia ya elimu, huduma rafiki kwa vijana, na kushughulikia vikwazo vya kijamii na kisheria.
Hapa nchini Mikoa ya Lindi na Mtwara imepunguza viwango vya mimba za utotoni kutoka asilimia 42 mwaka 2015/16 hadi asilimia 25 mwaka 2022, kutokana na elimu ya afya ya uzazi kwa vijana.
lakini hali bado ni tofauti katika Mikoa inayoongoza kwa mimba za utotoni ni Songwe (45%), Ruvuma (37%), Katavi (34%), Mara (31%), na Rukwa (30%).