Dodoma FM
Dodoma FM
30 April 2025, 6:03 pm

Mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 544 laki mbili ishirini na tano mia sita ishirini na sita (544, 225, 600) kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu.
Na lilian Leopord.
Ujenzi wa Shule mpya ya Sekondari Matumbulu umetajwa kutatua changamoto ya wanafunzi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma ya elimu.
Akisoma taarifa ya mradi, Mlezi wa Shule Mwalimu Zedekia Agutu amesema mradi huo utakamilika mwezi Mei 2025, na mpaka sasa baadhi ya wanafunzi wameshaanza masomo.

Naye Diwani wa Kata ya Matumbulu, Emmanuel Chibago ameiomba halmashauri kurekebisha barabara ili wanafunzi waweze kufika shuleni kiurahisi.
Kwa upande wake Daud Mkhandi Kiongozi wa Kamati ya Fedha na Utawala amebainisha mipango yaliyoiweka katika kuhakikisha shule hiyo inakua na usalama.