Waganga na wakunga watiba asilia watakiwa kujua sheria ili kuepusha migogoro kwa jamii
28 June 2021, 11:26 am
Na; Benard Filbert.
Imeelezwa kuwa uelewa mdogo wa sheria kwa waganga wa tiba za asili nchini ni sababu inayo pelekea kutokea kwa migogoro mingi katika jamii.
Hayo yameelezwa na katibu wa umoja wa waganga na wakunga asilia nchini Bwana Lucas Mlipu wakati akizungumza na taswira ya habari juu ya uelewa mdogo na sheria kwa Wagaga wa Tiba asili.
Bwana Mlipu amesema wamegundua waganga wengi wa tiba asili nchini hawana uelewa wa sheria za ufanyaji wa kazi.
Pamoja na changamoto hiyo amesema toka waanze kutoa elimu kwa waganga wa tiba asili kumekuwa na mabadiliko makubwa ikiwemo kupungua kwa migogoro ambayo ilikuwepo hapo awali.
Baadhi ya wananchi wakizungumza na taswira ya habari wamesema kuna umuhimu wa waganga wa tiba asili kuzitambua sheria ambazo zitasaidia kufanya kazi kwa maadili.
CLIP WANANCHI……………….03
Waganga wa tiba asili wanapaswa kufuata sheria ili kupunguza migogoro katika jamii.