Wanafunzi watakiwa kuacha kujihusisha na mapenzi
28 March 2022, 3:14 pm
Na; Neema Shirima.
Wanafunzi wa kike wameshauriwa kuachana na kujihusisha na mapenzi ili kuepuka kupata magonjwa mbalimbali ya zinaa kama vile ukimwi
Haya yamezungumwa ikiwa imesalia mwezi mmoja wanafunzi wa kidato wa sita kufanya mitihani yao ya mwisho ya kuhitimu elimu ya sekondari.
Ushauri huo umetolewa na mbunge wa viti maalumu mkoa wa Dodoma bi Fatma Tawfiq wakati akizungumza na wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika viwanja vya shule ya sekondari ya Dodoma hapo jana katika uzinduzi wa clabu ya sikio la kike ambapo amewashauri wazingatie masomo wanapojiandaa kwenda kujiunga na vyuo mbalimbali
Nae bi Zainab Bakari ambae ni mkurugenzi wa clab ya sikio la kike Tanzania amesema lengo la kuanzisha clab hiyo ni kuzunguka baadhi ya shule na kuzungumza na wanafunzi wa kidato cha tano na sita na kuwashauri kuhusu maisha watakayoenda kuyaanza na namna ya kuepukana na changamoto mbalimbali baada ya kumaliza elimu ya sekondari
Aidha kwa upande wa wanafunzi wameishukuru taasisi ya clab ya sikio la kike kwani kupitia club hiyo wameweza kujifunza shughuli mbalimbali kama vile kutengeneza keki na kujifunza kuendeleza vipaji walivyo navyo
Jamii na taasisi mbalimbali zinashauriwa kujitolea katika kutoa elimu juu ya maisha baada ya shule ya sekondari ili waweze kufahamu namna watakavyoweza kukabiliana na changamoto za mitaani pamoja na vyuoni