Sambwa ,Kondoa walia na changamoto ya kukosa Zahanati
7 May 2021, 12:05 pm
Na; Benard Filbert.
Wakazi wa Kijiji Cha Sambwa Kata ya KK Wilayani Kondoa wamelalamikia ukosefu wa huduma za afya katika Kijiji hicho hali inayowalazimu kutembea umbali mrefu kwa ajili ya matibabu.
Bw.Ally Khamis ni mkazi wa Kijiji hicho amesema wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za afya kutokana na kata hiyo kukosa Zahanati.
Ameongeza kuwa licha ya kukutana na changamoto hiyo bado hakuna dalili za kusogezewa huduma hiyo karibu ili wapate matibabu kwa urahisi.
Bwana Ally Omary ni mwenyekiti wa Kijiji cha Sambwa amesema ni kweli katika hiyo hakuna Zahanati ila tayari wamekaa vikao na viongozi wote wa Kata na hivi karibuni wanatarajia kuanza kukusanya michango kutoka kwa wananchi ili kuanza ujenzi wa zahanati.
Huduma za afya ni muhimu kwa binadamu licha ya baadhi ya Vijiji nchini kukosa kabisa Zahanati hivyo kutembea umbali mrefu kutafuta huduma hizo.