Elimu zaidi yahitajika kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia
30 October 2024, 6:29 pm
Mariam Matundu.
Imeelezwa kuwa ni muhimu
Jamii inatakiwa kufahamu na kuelewa utaratibu wa kuripoti matukio ya ukatili wa kijinsia ili kuwezesha kuripotiwa kwa kesi hizo na kufanyika ufuatiliaji.
Akizungumza katika mdahalo wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana Dodoma ulioandaliwa na shirika la AFNET, Kamishna Msaidizi wa Polisi ambaye ni Afisa Polisi Jamii Mkoa wa Dodoma Bi. Eva Stesheni amesema kuwa kesi nyingi zinaharibika kwa kutokutoa ushahidi .
Aidha Bi Eva Stesheni amesema kuwa jeshi la polisi kupitia kampeni mbalimbali linaendelea kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia ambayo imeleta manufaa makubwa katika mapambano ya ukatili ndani ya mkoa wa Daodoma.
Mdahalo huo umeandaliwa na shirika la AFNET kwa ufadhili wa shirika la WOMEN FUND TANZANIA TRUST umehudhuliwa na wadau mbalimbali wa maendeleo . Octoba 29, 2024 jijini Dodoma.