Akina mama wanaonyonyesha watakiwa kuripoti wanaponyimwa muda
12 August 2024, 4:19 pm
Kwa mujibu wa Sheria ya Kazi na Ajira ya mwaka 2004 kifungu cha 33 (10) kinatoa haki kwa mama aliyejifungua kwenda kunyonyesha mtoto saa 2 hadi miezi sita baada ya kutoka likizo ya uzazi kulingana na makubaliano na waajiri.
Na Yussuph Hassan.
Wito umetolewa kwa akina mama wanaonyenyosha katika sekta rasmi na zisizo rasmi endapo wakinyimwa nafasi ya kwenda kunyonyesha watoto kulingana na masaa waliyokubaliana na waajiri kutoa taarifa ili sheria ifuate mkondo wake.
Wito huo umetolewa na mwanasheria kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binaadamu Euphrasi Peragius wakati akizunguma na Dodoma TV.
Kwa upande wao baadhi ya Wafanyakazi wamesema kwa sasa Waajiri wamekuwa wakiwapa haki hiyo akina Mama wanaonyonyesha.
Semenieva Juma ni Afisa Lishe Jijini Dodoma Grace amesema unyonyeshaji Maziwa ya Mama ni njia bora na salama ya kulisha Watoto.