Dodoma FM
Dodoma FM
3 December 2025, 12:43 pm

Changamoto hiyo ni kubwa Kwa wakazi wa Igandu kwani inakwamisha baadhi ya shughuli za kijamii. Picha na Mtandao.
Aidha amesema amejitahidi kuwasilisha maombi kwa wakandarasi wanaofanya ukarabati kwenye maeneo ya kalavati Ili kuwajengea kivuko katika reli hiyo.
Na Victor Chigwada.
Kukosekana kwa vivuko katika reli ya mwendokasi SGR imekuwa kikwazo Kwa wakazi wa Kijiji cha Igandu Wilaya ya Chamwino jambo linaokwamisha shughuli za wananchi na wanafunzi pindi wanapo hitaji kuvuka upande wa pili.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Igandu Bi.Joyce Chiloweka anasema changamoto hiyo ni kubwa kwa wakazi wa Igandu kwa inakwamisha baadhi ya shughuli za kijamii.
Bi.Chiloweka ameiomba Serikali kupitia shirika la reli nchini kuboresha eneo hilo kwa kujenga vivuko kwani wapo watoto wenye ulemavu ambao wanashindwa kupita kwenye makalavati Ili kwenda shuleni.
Nao baadhi ya wananchi kijijini hapo wamezungumzia kukoseka kwa vivuko na kalavati kunavyo waathiri katika shuguli zao hasa wanapo lazimika kuvuka.