Dodoma FM

Wataalam wapendekeza karanga kwa afya ya moyo, ubongo

1 December 2025, 12:37 pm

Tafiti za lishe zinaonyesha kuwa ulaji wa karanga unaweza kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo kwa asilimia 15, na pia kuchangia katika kuimarisha kinga ya mwili. Picha na Mtandao.

Mbali na kuwa kitafunwa cha kawaida, karanga huchangia kuongeza kinga ya mwili na kuboresha utendaji kazi wa mwili kwa ujumla, ikiwemo kupunguza uchovu na kuimarisha misuli.

Na Lilian Leopold.

Wataalam wa afya wamebainisha kuwa karanga ni chanzo muhimu cha virutubisho vinavyosaidia kuimarisha afya ya binadamu, hususan kutokana na uwepo wa vitamin E na madini ya magnesium.

Afisa Lishe kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Beatrice Moshi, amezungumza na Taswira ya Habari kuhusu virutubisho vinavyopatikana kwenye karanga na umuhimu wake kwa binadamu.

Sauti ya Beatrice Moshi.

Kwa upande wake Amani Meena, mwanafunzi wa Udaktari kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, amesema ulaji wa karanga unaweza kuongeza uwezo wa kumbukumbu na kuimarisha utendaji wa ubongo kutokana na virutubisho vinavyopatikana ndani yake.

Sauti ya Amani Meena.

Kuhusu aina ya karanga zinazofaa kuliwa, wataalamu hao wanashauri karanga zilizokaangwa bila mafuta mengi au mbichi, kwani huhifadhi virutubisho vyake kwa kiwango kikubwa.

Sauti ya Beatrice Moshi na Amani Meena.

Hata hivyo, wataalamu wanatoa wito kwa  wananchi wenye uzio wa karanga kujiepusha kabisa na ulaji wake, huku wakitoa tahadhari kwa watu wenye uzito uliopitiliza na wale wenye shinikizo la damu kuwa makini na matumizi ya karanga kutokana na kiwango kikubwa cha mafuta kilichomo.