Dodoma FM
Dodoma FM
25 November 2025, 3:22 pm

Ikumbukwe kwua Kazi ya ukusanyaji taka rejeshi imeelezwa kuwa ni sehemu muhimu ya uhifadhi wa mazingira na chanzo cha mapato kwa watu wengi, hivyo jamii inapaswa kuondoa dhana hasi na kutambua mchango wa wahusika wa kazi hiyo.
Na ;Anwary Shaban.
Jamii imetakiwa kuwapa heshima na thamani watu wanaojishughulisha na kazi ya kuokota taka rejeshi katika maeneo mbalimbali, kwani kazi hiyo ni chanzo muhimu cha kipato.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi Edwad Joakim kutoka kiwanda kidogo cha David Risaikobin Services kilichopo maeneo ya Mwatano jijini Dodoma, akisema waokota taka rejeshi wamekuwa na mchango mkubwa katika uchumi wa kaya na kuhakikisha mazingira yanabaki salama.
Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Mazingira ya Tanzania (1997, marekebisho 2021), Serikali inatambua umuhimu wa usimamizi wa taka na kuchakata taka rejeshi kama sehemu ya mkakati wa kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuongeza ajira.
Bw Joackim anasema licha kazi hiyo kuonekana muhimu lakini, bado watu hao hukumbana na changamoto lukuki ikiwemo ukosefu wa vifaa vya kujikinga na mazingira magumu ya kazi.
Taswira ya Habari pia imezungumza na mmoja wa waokota taka rejeshi jijini Dodoma, Teresia Daniel, ambaye ameeleza namna kazi hiyo imekuwa sehemu muhimu ya kuendesha maisha yake ya kila siku.
Hatua hii ni utekelezaji wa Mpango wa Dunia wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), hususan Lengo namba 12: Matumizi na Uzalishaji Endelevu, unasisitiza kupunguza taka na kuongeza urejelezaji ili kulinda mazingira na afya za binadamu.
Baadhi ya wananchi wamesema kuwa watu wanaojihusisha na kazi hiyo huchangia kwa kiasi kikubwa kuweka mazingira safi, huku pia wakijipatia kipato kutokana na shughuli wanazofanya na kuifanya kuwa sehemu ya uchumi wa maeneo yao.