Dodoma FM

Wanawake waathirika zaidi ukatili mtandaoni

17 October 2025, 12:19 pm

Ripoti ya LHRC ya mwaka 2023 imebainisha ongezeko la ukatili wa kijinsia mtandaoni nchini hasa kwa wanawake. Picha na INEC.

Ongezeko la ukatili wa kijinsia mtandaoni limeibua mjadala mpana kati ya vijana na wataalamu kuhusu hatua za kuchukua kuondoa vitendo hivyo wakati wa kampeni za uchaguzi.

Na Mariam Matundu.

Ripoti ya kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC ya mwaka 2023 inaonesha kuwepo kwa ongezeko la udhalilishaji wa kidijitali na ukatili wa kijinsia mtandaoni nchini huku wanawake wakiwa walengwa kwa asilimia 56.

Hata hivyo zipo sheria zinazopinga vikali ukatili wa kijinsia wakati wa uchaguzi ikiwemo sheria ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani. Sheria ya Vyama vya Siasa na Sheria ya Tume Turu ya Taifa ya uchaguzi zote za mwaka 2024.

Tumefanya mjadala na vijana na wataalamu kuhusu suala hili tukiuliza unaondoaje vitendo vya ukatili wakati wa kampeni za uchaguzi?

Mjadala kuhusu ukatili kwa wanawake.