Dodoma FM
Dodoma FM
15 October 2025, 12:27 pm

Ukatili unaofanywa na wazazi kwa watoto umechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa idadi ya watoto wanaoishi kwenye vituo vya malezi.
Na Selemani Kodima.
Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wanawake na makundi maalumu imesema itaendelea kuwachukulia hatua za kisheria dhidi ya familia,wazazi na jamii kwa ujumla wanaofanya vitendo vya kikatili dhidi ya watoto.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Ustawi wa Jamii ambaye pia Meneja wa Kituo cha Makao ya Taifa ya Kituo cha kulelea watoto Kikombo mkoani Dodoma Darius Kalijongo, alipokuwa akizungumza siku ya kumbukumbu ya Baba wa Taifa hayati Mwalimu Nyerere inayofanyika kila mwaka Oktoba 14.
Kalijongo amesema kuwa kuongezeka kwa watoto hao kwenye vituo mbalimbali hapa nchini kunachangia kwa kiasi kikubwa na wazazi,familia na jamii kwa ujumla, kutokana na kutoshiriki katika kuwapatia haki zao za msingi hali ambayo imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa kujikuta wakifanyiwa vitendo vya kikatili
Amesema kuwa kutokana na hali hiyo Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kamwe hatawafumbia macho kwa watakaohusika katika kuwafanyia vitendo hivyo vya kikatili dhidi ya watoto hao ambao wakipatia haki zao kunaweza kuwa faida kwa upande wa jamii,wazazi pamoja na familia wanazotoka.

Aidha amewataka wazazi,walezi,jamii na wadau mbalimbali kuwakumbuka watoto ambao wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu,kwa kuwpati misaada mbalimbali ikiwemo upendo,furaha na ushirikiano wa karibu wa vitendo ili na wao wajionee ni sehemu ya watu wanaohitajika kuleta mchnago wao wa kimandeleo ndani ya Taifa.
“Kituo chetu kina jumla ya watoto wote 197 na hapa tumekuwa tukifandisha masomo mbalimbali yakiwemo ya kufanya kazi kwa bidii ,ujasirimali na fani za michezo,ili watakapotoka waweze kuwa na faida kwenye familia zao na wao wenyewe pamoja na jamii inayowanzunguka”.amesema.
Awali wakizungumza kwenye kituo hicho watoto hao wameiomba kufundishwa historia ya Taifa juu ya viongozi mbalimbali kwa waliopita ili waweze kujengea misingi bora itakayowafanya kuiga na kuendelea kuelimisha kwa vizazi vijavyo.
“Tunaiomba serikali kupitia wahusika wake watupatie elimu ya historia ya wasisi wa nchi yetu ambao waliopita ili waweze kutujenga kuijua historia ya viongozi wetu,hii itasaidia watoto walio wengi kuwatambua kwa vitendo kuhusu kazi walizokuwa wakizifanya kwa ajili ya Taifa letu”. wamesema.

Naye Mchungaji Benadina Nyoni wa Kanisa la Calvair Assembles of God akizungumza na waandishi wa habari kwenye kumbukumbu hiyo ya hayari Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alisema kuwa kuongezeka kwa watoto wa mitaani kunatokana na ukosefu wa misingi bora ya malezi ya kiroho na kijamii kutoka kwa wazai walezi na jamiii.
Mchungaji huyo alitaja changamoto nyingine inachochangia pia ni kwa baadhi ya wazazi na walezi kuwanyoshea vidole watoto na wengine kufikia hatua ya hata ya kuchomwa na matairi kutokana na kukosa kwa misingi ambayo ingeweza kuwasaidia kuondokana na maisha ya kuishi mitaani bila msaada wowote wa limaadili ya kiroho.