Dodoma FM

Kibano watumishi wasiowajibika kazini

24 April 2025, 5:56 pm

Mfumo huo umeanzishwa mahususi kupima viashiria vya utendaji kazi (KPI) kwa kila mtumishi.Picha na Google.

Watumishi watakaoshindwa kufikia kiwango hicho hawatapandishwa vyeo wala kuongezewa mishahara.

Na Mariam Kasawa

Serikali imetangaza mkakati wa kuwachukulia hatua kali watumishi wa umma wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo, ikiwemo kutowapandisha madaraja wala kuongeza mishahara yao.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi, Aprili 24, 2025, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu, wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee.

Mdee alitaka kufahamu mpango wa Serikali katika kukabiliana na takriban asilimia 40 ya watumishi wa umma wanaodaiwa kutotekeleza majukumu yao ipasavyo licha ya kulipwa mishahara.

Ameeleza kuwa mfumo huo umeanzishwa mahususi kupima viashiria vya utendaji kazi (KPI) kwa kila mtumishi, ambapo kiwango cha chini cha ufaulu kimewekwa kuwa asilimia 60.

clip maswali na majibu.