Dodoma FM

Taka za kielektroniki ni fursa na ajira

12 August 2024, 3:51 pm

Picha ni taka za kielectroniki zikiwa zimetupwa.Picha na UN news.

Shirika la Kazi Duniani, ILO linasema licha ya uzalishaji mkubwa wa taka hizo za kielektroniki ni asilimia 20 tu ya tani hizo za kielektroniki ndio hurejelezwa katika mazingira rasmi.

Na Mariam Kasawa.
Inaelezwa kuwa taka za kieletroniki zinazo zalishwa na kutupwa katika mazingira kila siku zinaweza kuchakatwa na kurejeleshwa ili zitumike katika mifumo mingine.

Kwa mujibu wa Shirika la kazi duniani, ILO linataka hatua za haraka zichukuliwe ili kusimamia vyema taka za kielektroniki zinazozalishwa kote ulimwenguni ili hatimaye ziwe chanzo cha ajira zenye utu.

wafanyakazi na waajiri wamesema wakati umefika kwa serikali kuwekeza zaidi kwenye mifumo ya kuchakata na kutumia upya taka za kielektroniki kwa kuzingatia kasi kubwa ya ongezeko la taka hizo ambazo kila mwaka huzalishwa tani milioni 51 zikiwa na thamani ya dola bilioni 62.

Bw. Taimuru Kissiwa meneja wa utekelezaji sheria kutoka NEMC anasema taka za kieletroniki ni mali kama zilivyo taka za plastiki kwani zinaweza kurejeshwa na kutumika katika mifumo mingine.

Taka hizi zinapaswa kuhifadhiwa vizuri na kutupwa sehemu husika.Picha na Google.

Afisa mzingira mwandamizi kutoka Nemc Bi. Kuluthumu shuhu anawahimiza wananchi kuendelea kutunza mazingira kwa kuhakikisha taka hasa taka za kieletroniki zinahifadhiwa sehemu salama.

Tanzana inakabiliwa na ongezeko la taka za kieletroni kwa kuzalisha tani milioni 51 kila hii inachangiwa na kukosekana kwa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi na kuto zifahamu sera za mazingira zinasema nini.

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis anasema wapo katika mikakati ya kuangalia ni namna gani taka hizi zinaweza kupunguza pamoja na kuwaeleza wananchi namna bora ya kupunguza taka hizi katika mazingira.