BRELA, FCC zatajwa kuchochea maendeleo sekta ya viwanda na biashara
12 February 2024, 3:24 pm
Wakala wa usajili wa biashara na leseni Tanzania (BRELA) na Tume ya ushindani Tanzania (FCC)zimekutana na kamati ya kudumu ya Bunge ya viwanda ,Biashara ,kilimo na Mifugo kutoa semina ya nana taasisi hizo zinatekeleza majukumu yao na kuleta mchango katika kuchochea maendeleo .
Na Mariam Matundu .
Wakala wa usajili wa biashara na leseni Tanzania (BRELA) na Tume ya ushindani Tanzania (FCC)zimetajwa kuwa taasisi muhimu katika kuchochea na kukuza maendeleo katika sekta mbalimbali hususani biashara na viwanda.
Kauli hiyo imetolewa na naibu waziri wa viwanda na biashara Mhe. Exaud Kigahe katika kikao kati ya taasisi hizo mbili pamoja na kamati ya kudumu ya Bunge Viwanda ,Biashara ,Kilimo na Mifugo ambapo naibu waziri amezitaja taasisi hizo kama kiungo muhimu katika maendeleo.
Aidha ameitaka BRELA kuendelea kurahisisha mchakato wa kujasili kampuni na kutoa elimu kwa wafanyabiashara ya umuhimu wa kurasimisha biashara zao pia amesisitiza FCC kuendelea kudhibiti bidhaa bandia ili kukuza sekta binafsi.
kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya viwanda ,Biashara ,mifugo na kilimo Deo Mwanyika amesema kamati imeridhishwa na ufanisi wa utendaji kazi wa taasisi ya BRELA NA FCC na kwamba amepongeza taasisi hizo kwa kutoa uelewa kwa kamati ambao ni wawakilishi wa wananchi.
Mkurugenzi mkuu wa FCC William Erio amesema tayari mchakato wa maboresho ya sheria ya ushindani umeanza ili kuendana na wakati huku Afisa mtendaji mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa amesema tangu kuanza kutumia mfumo kusajiri kampuni imesaidia kupunguza muda ambapo kwa sasa ndani ya siku mbili mchakato unakamilika.